Ayatullah Hashemi Rafsanjani ameongeza kuwa, moja ya vigezo muhimu vya jamii yenye itibari duniani ni kiwango cha ushiriki katika uchaguzi. Akihutubia maelfu ya waumini katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran, Ayatullah Rafsanjani amesema maadui wa mfumo wa Kiislamu ambao kwa ajili ya uhasidi na chuki wanataka kuibua ufa baina ya wananchi na viongozi wa mfumo, watapata pigo baada ya kushuhudia idadi kubwa ya wananchi watakaoshiriki katika uchaguzi wa 10 wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hatibu wa sala ya Ijumaa amesisitiza kuwa, bila kuwepo irada na kushiriki wananchi, serikali ya Kiislamu haiwezi kufikia malengo yake.
Ayatullah Rafsanjani ameashiria safari ya siku nane ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika mkoa wa Kurdistan wa Iran na mapokezi makubwa aliyopata kutoka kwa wananchi wa eneo hilo. Amesema safari hiyo sawa na safari nyinginezo za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu itakuwa na athari zenye baraka nyingi kwa Iran na Ulimwengu wa Kiislamu. Ayatullah Rafsanjani ameashiria sisitizo la Kiongozi Muadhamu kuhusu umoja wa Waislamu na kusema, balaa kubwa leo katika ulimwengu wa Kiislamu ni mifarakano, jambo ambalo halijakuwa na natija yoyote isipokuwa hasara kwa Ummah.409052