Kongamano hili limeandaliwa kwa ushirikiano wa Jamhuri ya Baskorostan katika Shirikisho la Russia na Kituo cha Utafiti wa Historia, Sanaa na Utamaduni wa Kiislamu IRICA chenye makao yake Istanbul Uturuku.
Kongamano hilo litajadili historia ya ustaarabu wa Kiislamu katika eneo la Volga-Ural. Kati ya masuala yatakayojadiliwa ni sayansi, filosofia, teknolojia, sanaa, lugha, fasihi na sekta nyinginezo za kielimu. Kongamano hilo pia litajadili nafasi ya ustaarabu wa Kiislamu katika eneo hilo katika miaka ya huko nyuma na nafasi ya Uislamu katika kuimarisha utamaduni wa mazungumzo baina ya wakazi wa eneo hilo.
Washiriki katika kongamano hilo wanaweza kuwasilisha makala zao kwa lugha za Bashkir, Kirusi na Kiingereza. 555096