Kongamano la kimataifa la "Uislamu na Elimu za Kiakili, Zama Zilizopita na Sasa" limenza kazi zake katika mji mkuu wa Algeria Algiers likihudhuriwa na wasomi na wataalamu kutoka nchi mbalimbali duniani.
Kongamano hilo la siku tatu limetayarishwa na Baraza Kuu la Waislamu wa Algeria. Kongamano hilo linajadili masuala yanayohusiana na ustaarabu wa Kiislamu katika karne za kati hususan zama za utawala wa Bani Abbas na ustawi wa elimu za kiakili katika kipindi hicho.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu wa Algeria Sheikh Bu Imran amesema kongamano hilo linafanyika kwa lengo la kujibu maswali yanayotolewa na baadhi ya wanafikra kuhusu kiwango cha uwiano uliopo baina ya Uislamu na akili na hisa ya dini hiyo tukufu katika kuustawisha ustaarabu duniani.
Sheikh Bu Imran amesema baadhi ya watafiti, wasomi na wataalamu hususan katika nchi za Magharibi wana shaka na ufahamu usiokuwa sahihi kuhusu kiwango cha mazingatio ya Uislamu kwa elimu za kiakili na sayansi kutokana na maarifa yao finyu kuhusu utamaduni wa Kiislamu; kwa msingi huo kuna udharura wa kepewa majibu katika uwanja huo.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu wa Algeria amesisitia kuwa Qur'ani Tukufu na Suna za Mtume (saw) zimesisitiza mno juu ya udharura wa kutafuta elimu na kufanya uhakiki katika elimu za kiakili na kifikra. 555832