Mtandao huo unaoungwa mkono na Wazayuni unazalisha na kuuza mavazi yanayokuwa na maandishi au nembo zinazovunjia heshima matukufu ya Kiislamu, Waislamu na Mwenyezi Mungu. Bidhaa zinazozalishwa na mtandao huo huuzwa kwa wingi kwa lengo la kuwaunga mkono Wazayuni.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa mwaka jana jumuiya moja ya Kikristo katika jimbo la Florida nchini Marekani lilisambaza na kuuza tisheti zenye maandishi yanayovunjia heshima matukufu ya Kiislamu, hatua ambayo ilipingwa vikali na jumuiya za Kiislamu katika nchi mbalimbali. 625887