IQNA

Mipango ya Kiutamaduni ya Mashindano ya Kimataifa ya Quran ya Dubai

9:43 - August 08, 2010
Habari ID: 1968791
Mipango ya Kiutamaduni pembizoni mwa Mashindano ya 14 ya Kimataifa ya Quran Tukufu ya Dubai imetangazwa.
Kwa mujibu wa gazeti la gazeti la Khaleej Times Mkuu wa Kamati ya Uandalizi wa Maonyesho hayo Ibrahim Bu Melha amesema: “Pembizoni mwa Zawadi ya Dubai (Mashindano ya Kimataifa ya Quran ya Dubai) kutakuwa na hotuba 28 zenye maudhuri ya Quran Tukufu. Hotuba 25 zitakuwa kwa lugha ya Kiarabu, hotuba mbili kwa lugha ya Malayu na hotuba moja kwa lugha ya Bengali”. Hotuba hizo zitakuwa zikianza saa nne na robo usiku kwa wakati wa Dubai katika maeneo mbali mbali mjini humo.
Bu Melha ameongeza kuwa kati ya walioalikuwa kuzungmza ni Sheikh Yusuf Juma Islam, Imamu wa Msikiti wa Al Aqsa.
Mashindano ya 14 ya Kimataifa ya Quran Tukufu ya Dubai yataanza tarehe 8 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
627759
captcha