Habari za kuaminika zinasema kuwa makumbusho hayo yameandaliwa na jumuiya ya Marafiki wa Kalamu wa mji wa Qatif na kwamba wasomi, wanafikra, maulama pamoja na wakazi wa mji huo wametangaza kuwa watashiriki kwa wingi katika makumbusho hayo. Jumuiya hiyo imetangaza kwamba makumbusho hayo yataanza saa tatu usiku kwa wakati wa Saudi Arabia na kwamba wasomi watakaoshiriki watatoa hotuba tofauti wakibainisha na kufafanua shakhsia na fikra za Allamah Fadhlullah. Allamah Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah aliaga dunia tarehe Nne Julai katika Hospitali ya Bahman ya mjini Beirut Lebanon akiwa na umri wa mika 74 kutokana na uvujaji damu wa ndani.628095