Ikitangaza ratiba hizo jumuiya hiyo imeziomba taasisi na mashirika ya uwakilishi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Paris pamoja na wanachuo wa Kiirani na wa nchi nyinginezo wanaoishi katika mji huo kushiriki katika vikao na ratiba hizo za mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kusimamishwa swala za jamaa, kutolewa futari, kusomwa dua ya Kumeil usiku wa kuamkia Ijumaa, sherehe za kuzaliwa Imam Hassan Mujtaba (AS) tarehe 26 Agosti pamoja na amali za kuhuisha mikesha ya tarehe 19, 21 na 23 ya mwezi wa Ramadhani ni miongoni mwa mipango na ratiba za jumuiya hiyo katika mwezi huu mtukufu.
Jumuiya ya Wapenzi wa Zahra (AS) imetangaza kuwa siku ya Alkhamisi tarehe 12 Agosti itakuwa siku ya kwanza ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani. 628535