IQNA

Chuo Kikuu cha London, mwenyeji wa kikao cha kimataifa cha Beitul Muqaddas

10:35 - August 09, 2010
Habari ID: 1969618
Kikao cha 12 cha kimataifa kuhusu Beitul Muqaddas kitafanyika tarehe 6 Novemba katika Chuo Kikuu cha London.
Kwa mujibu wa tovuti ya Isra kikao hicho ambacho kitafanyika chini ya anwani ya 'Utafiti wa Wataalamu wa Mashiriki ya Kati kuhusu Beitul Muqaddas' kitafanyika katika Chuo cha Utafiti wa Mashariki na Afrika. Kikao hicho kimeandaliwa na Chuo cha Utafiti wa Beitul Muqaddas ISRA. Kikao hicho kitaandaliwa kwa shabaha ya kuchunguza na kutalii utafiti uliofanyika duniani kuhusiana na Beitul Muqaddas na umuhimu wake kwa Waislamu, kuleta muamko, kuimarisha heshima ya pande mbili, maelewano, mazungumzo na ushirikiano kati ya taasisi na jumuiya za Kiislamu na zisizo za Kiislamu kuhusu suala hilo.
Mitazamo ya watafiti wa Mashariki ya Kati, Utafiti na misingi ya utafiti kuhusu Beitul Muqaddas, mtazamo wa Uislamu na Waislamu kuhusu watafiti wa Mashariki ya Kati na Umuhimu wa Beitul Muqaddas kwa Waislamu ni miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa katika kikao hicho.
Chuo cha Utafiti wa Beitul Muqaddas ambacho awali kilikuwa kikiitwa Chuo cha Utafiti wa Kiislamu kiliasisiwa mwaka 1996 mjini London kwa madhumuni ya kutafiti masuala yanayohusiana na eneo hilo tukufu la Kiislamu. 628698
captcha