Mwandishi na jarida hilo Sara Hafidh amesema kuwa lengo lake kuu ni kutoa mafunzo ya Kiislamu kwa lugha nyepesi kwa watoto wadogo. Amesema kuwa ni muhimu kwa watoto wa Kiislamu wanaoishi katika nchi za Ulaya kujifaharisha kwa Uislamu wao na suala hilo haliwezekani bila ya kupata elimu na mafunzo.
Sara Hafidh ameongeza kuwa iwapo watoto wa Kiislamu watatambua thamani za dini yao na kuelewa jinsi dini ya Kiislamu inavyojali maadili ya mtu binafsi na jamii, kamwe hawawezi kupotea njia ya haki na sahihi.
Miongoni mwa masuala yatakayochapishwa katika jarida hilo ni pamoja na visa vifupi vya Mtume Muhammad (saw), picha zinazohusu maudhui za Qur'ani na za kidini, makala za kisayansi na Kiislamu na kadhalika.
Jarida hilo limeanza kutangazwa katika mitandao mingi ya Kiislamu kwenye intaneti. Unaweza kusoma jarida hilo kwa kutumia anwani ifuatayo: http://www.minimuslimeen.com 628743