IQNA

Kitengo cha vijana katika maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani

7:42 - August 10, 2010
Habari ID: 1970259
Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayofanyika mjini Tehran yana kitengo maalumu cha vijana kinachotoa mafunzo mbalimbali ya Qur'ani Tukufu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, vijana wanaofika katika kitengo hicho wanapata majibu ya maswali yao kuhusu masuala ya itikadi. Wataalamu wa kidini walio hapo wanatoa majibu katika mazingira ya kirafiki na kwa kuzingatia mahitajio ya vijana.
Aidha kati ya mafunzo mengine yanayotolewa hapo ni mafundisho ya sanaa na kaligrafia ya aya za Qur'ani Tukufu.
Kitengo hicho vile vile kinatoa mafunzo kwa vijana kuhusu kuandika weblogu za Kiislamu na kutoa zawadi kwa waandishi bora zaidi.
Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran yanafanyika katika ukumbi wa sala wa Imam Khomeini na yataendelea hadi tarehe 23 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Maonyesho hayo pia yana washiriki kutoka nchi 25 duniani.
629986
captcha