Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kikao hicho kitafanyika kwa mnasaba wa mwaka 2010 ambao umetangazwa na Shirika la Masuala ya Dini la Uturuki kuwa ni “ Mwaka wa Qur'ani Tukufu”. Kikao hicho kitahudhuriwa na wasomi Waislamu na wananchi.
Kikao hicho kati ya mengine, kitajadili nafasi ya visa vya Qur'ani katika maisha ya kila siku ya Waislamu na njia za kuitetea Qur'ani Tukufu.
Metin Uçar na Hüseyin Yavuz ni kati ya waandishi na wasomi wa kidini nchini Uturuki watakaojiunga na Maulama wa Kiislamu katika kikao hicho.
633551