Kwa mujibu wa gazeti la Uturuki la Hurriyet, maonyesho haya ya kimataifa yanafanyika kwa himaya ya Jumuiya ya Waqfu wa Sayansi, Teknolojia na Utamaduni wa Uturuki katika eneo lenye ukubwa wa mita elfyu moja mraba. Katika maonyesho hayo, uvumbuzi wa Waislamu kutoka karne ya saba hadi kumi na saba Miladia utaonyeshwa kama nembo ya turathi ya utamaduni wa Kiislamu.
Itakumbukwa kuwa wakati Waziri Mkuu wa Uturuki Rajab Tayyib Erdogan alipotombelea maonyesho ya “Zama za dhahabu za Uislamu, Uvumbuzi 1001” mjini London mwezi Machi aliandaa mazingira ya kufanyika maonyesho makubwa zaidi kama hayo katika mji wa Istanbul. Maonyesho sawa na hayo pia yatafanyika mjini New York mwezi Septemba.
636285