IQNA

Warsha ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika eneo la Buraida Saudi Arabia

11:24 - August 19, 2010
Habari ID: 1976642
Warsha ya Kuhifadhi Qur'ani inafanyika katika msikiti wa Aba Al-Halil katika mji wa Buraida mkoani Al Qasiim nchini Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Riyadh, warsha hiyo ilianza tarehe 11 Agosti kwa himaya ya Jumuiya ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu ya mji wa Buraida na itaendelea hadi tarehe 14 Septemba.
Warsha hii ni katika shughuli za Qur'ani Tukufu za Jumuiya ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu ya mji wa Buraida. Washiriki wa warsha hiyo wanajifunza mbinu za kuhifadhi Qur'ani Tukufu.
636648
captcha