Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, ensaiklopidia hiyo yenye juzuu 30 imekusanywa na Shahid Ashraf na kuchapishwa na Taasisi ya Chapa ya Anmol ya India. Kila moja ya juzuu hizo 30 ina anwani yake maalumu kuhusu maudhui inayojadiliwa ndani yake. Kati ya anuani muhimu za Ensaiklopidia hiyo ni pamoja na ufahamu wa utamaduni wa Kiislamu, utamaduni wa elimu katika Uislamu, mapinduzi ya utamaduni wa Kiislamu, utamaduni wa kisiasa katika Uislamu, utamaduni wa uchumi katika Uislamu, utamaduni wa amani katika Uislamu n.k.
Itakumbukwa kuwa Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran yalianza tarehe 27 Shaaban na yataendelea hadi tarehe 23 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
636558