Hayo yameripotiwa na gazeti la Imarati la al-Khaleej ambalo limesema kuwa washindi wa mashindano hayo yaliyofanyika katika makundi mawili ya wanawake na wanaume walishukuriwa na kupewa zawadi nono.
Akizungumza katika shehere hiyo, Nassir Hamdan az-Zaabi, mkuu wa Baraza la Uendeshaji wa Kituo cha Qur'ani cha Abu Dhabi ambaye pia ni mkuu wa Baraza la Wadhamini wa Zawadi ya al-Jabir amesema kuwa mashindano hayo hufanyika kila mwaka na kusimamiwa na Idara Kuu ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Imarati. Ameongeza kuwa kwa ujumla, washiriki 105 walishiriki katika mashindano hayo ambapo 53 walikuwa ni wanaume na 53 wanawake, walioshindana katika marhala tofauti za kuhifadhi Qur'ani. 636191