Kwa mujibu wa tovuti ya Batiweb, Maonyesho hayo ambayo yanafanyika kwa mnasaba wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani yatajumuisha athari za François Morel msanfifu majengo Mfaransa ambaye athari zake zinatokana na ilhamu ya usanifu majengo wa Kiislamu huko Uhispania, Mahdi Mutashar mchongaji mwenye asili ya Iraq na Redha Abidini, mtaalamu wa grafiki Muirani raia wa Uholanzi.
Mada ya maonyesho ya athari za Mahdi Mutashar itakuwa na anuani ya 'Sanaa za Kiislamu na Sanaa za Jiometria ya Magharibi'. Aidha Redha Abidini ataonyesho athari zake ambazo zimechukua ilhamu kutoka usanifu majengo wa Kiislamu wa Isfahan.
Katika maonyesho haya, Kitabu kijulikanacho kama Islamania kilichoandikwa na Véronique Rieffel Mkuu wa Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu cha Paris pia kitazinduliwa. 637375