Muhammad Abbas ameongeza kuwa jumba la makumbusho ya Kiislamu la Misri ambalo liliasisiwa mwaka 1899 limekuwa likikusanya turathi za Kiislamu kwa miaka mingi kwa shabaha ya kuzuia kuibiwa au kutoweka athari hizo. Amesema kuwa idadi ya athari hizo katika mwaka 1903 ilifikia turathi elfu saba.
Muhammad Abbas amesema kuwa jumba hilo la makumbusho lilifungwa mwaka 2003 kwa shabaha ya kukarabati na kuhesabu athari za kale na sanaa za mikono zilizoko ndani yake na kwamba sasa athari hizo zinafikia laki moja na elfu mbili.
Amesema kuwa kazi ya kukarabati jumba hilo la makumbusho ya Kiislamu imekamilika katika kipindi cha miaka 8 na limefunguliwa mwaka huu kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Baadhi ya athari za Kiislamu zinazohifadhiwa katika jumba hilo ni ufunguo wa dhahabu wa nyumba tukufu ya al Kaaba, dinari ya zamani zaidi ya Kiislamu iliyokuwa ikitumiwa katika karne ya kwanza Hijria, nakala kadhaa nadra zilizoandikwa kwa hati za mkono za Qur’ani Tukufu, mazulia ya Kiirani, vyombo vya udongo vya zama za utawala wa Kiothmani na kadhalika. 637919