Ensaiklopidia hiyo imetayarishwa na Zaky Kermani ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Sayansi na mhariri wa Jarida la Sayansi ya Kiislamu katika mji wa Alighar nchini India na Anki Singh, Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Taaluma ya Dini cha New Delhi. Ensaiklopidia hiyo imechapishwa na Global Vision Publication House nchini India.
Ensaiklopidia hiyo yenye juzuu nne imekusanya taarifa mbalimbali kuhusu taaluma za Kiislamu, historia ya maisha ya wasomi mashuhuri wa ulimwengu wa Kiislamu, shughuli zao za kielimu, itikadi na mitazamo yao ya kifalsafa na mchango wao katika ulimwengu wa sasa. Kitabu hicho pia kimechapisha picha za wasomi 382.
Ensaiklopidia hiyo ina kurasa 3208 na imendikwa kwa lengo la kuzidisha maarifa ya wasomaji wake kuhusu elimu na maarifa ya Kiislamu na wasomi wa Kiislamu. 638010