Ensaiklopidia hiyo imetayarishwa katika juzuu 10 na Muhammad Ilyas akishirikiana na M.H Sayyid ambao ni miongoni mwa wasomi wa Kiislamu wa India. Ensaiklopidia hiyo imechapishwa na kituo cha uchapishaji cha Anmol Publications.
Kila juzuu ya ensaiklopidia hiyo inabeba anwani ya maudhui maalumu na inajadili kwa mapana mafundisho ya Mtume wa Uislamu kuhusu maudhui hiyo.
Baadhi ya maudhui za ensaiklopidia hiyo ni: Mafundisho ya Nabii Mhammad (saw) na Mwenyezi Mungu na Takwa, Mafundisho ya Mtume Muhammad (saw) na Imani na Itikadi, Mafundisho ya Mtume Muhammad (saw) na Sayansi na Falsafa, Mafundisho ya Mtume Muhammad (saw) na Taasisi za Kiislamu, Mafundisho ya Mtume Muhammad (saw) na Elimu ya Maadili, Mafundisho ya Mtume Muhammad (saw) na Uhuru na Haki, Mafundisho ya Mtume Muhammad (saw) na Maisha ya Kila Siku, Mafundisho ya Mtume Muhammad (saw), Wanawake na Uhusiano wa Mke na Mume na Mafundisho ya Mtume Muhammad (saw) na Sheria za Kiislamu.
Ensaiklopidia ya Mafundisho ya Mtume Muhammad (saw) ina kurasa 3206 na imekusanya masuala mbalimbali kuhusu mafundisho ya Mtume huyo wa Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa maudhui zake kwa ajili ya kurahisha kazi kwa wasomaji.
Ensaiklopidia nyingine ambazo zinaonyeshwa kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya kimataifa ya Qur’ani mjini Tehran ni Ensaiklopidia ya Wasomi wa Kiislamu, Ensaiklopidia ya Utamaduni na Ustaarabu wa Kiislamu kwa lugha ya Kiingereza na Ensaiklopidia ya Ahlulbait (as) kwa lugha ya Kiarabu.
638898