IQNA

Kongamano la wanakaligrafia bora zaidi wa Qur'ani Imarati

12:39 - August 24, 2010
Habari ID: 1979764
Kongamano la wanakaligrafia bora zaidi wa Qur'ani katika nchi za Kiislamu litafanyika kuanzia tarehe 25 hadi 28 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani katika Umoja wa Falme za Kiarabu kwa lengo la kuandika kaligrafia ya msahafu kamili.
Kwa mujibu wa gazeti la Imarati la Al Itihad, kongamano hilo ambalo litafanyika kwa mwaka wa pili sasa litawajumuisha wanakaligrafia bora 30 kutoka nchi za Kiislamu na kila mmoja wao ataandika Juzuu moja ya Qur'ani kwa kaligrafia.
Kongamano hili linafanyika kwa himaya ya Wizara ya Utamaduni, Vijana na Ustawi ya Umoja wa Falme za Kiarabu.
Katika kongamano sawa na hili la mwaka jana wanakaligrafia wa Qur'ani kutoka maeneo yote ya ulimwengu wa Kiislamu waliandika msahafu kamili kwa mbinu bora zaidi za kaligrafia. 639926
captcha