IQNA

Jamiatul Mustafa (saw) kuanzisha vyuo vikuu vya kidini

11:19 - August 25, 2010
Habari ID: 1980899
Kutokana na kuongezeka idadi ya watu wanaoomba kupata maarifa ya Kiislamu kwa upande mmoja na uhaba wa vituo vya kidini katika kujibu na kutosheleza maombi hayo kwa upande wa pili, taasisi ya kimataifa ya Jamiatul Mustafa (saw) imepanga kueneza shughuli zake na kuanzisha vyuo vikuu vya kidini na taasisi za Qur'ani katika nchi mbalimabli za dunia.
Akizungumzia suala hilo katika mahijiano yake na shirika la habari za Qur'ani, IQNA, Sheikh Qassim, mkuu wa Taasisi ya Rasuul A'dham ya nchini Thailand amesema kuwa Jamiatul Mustafa (saw) ni kituo muhimu cha kimataifa cha elimu, ambacho kina nafasi maalumu katika ulimwengu wa Kiislamu na kwamba kinaweza kuwa na nafasi muhimu katika kueneza maarifa na mafundisho ya Qur'ani na kidini kwa Waislamu wote duniani.
Akiashiria kutajwa mwaka huu wa 1389 kwa mujibu wa kalenda ya Kiirani, na Hujjatul Islam Wal Muslimeen A'raafi, Mkuu wa Jamiatul Mustafa (saw) kuwa ni mwaka wa harakati ya kuimarisha shughuli za Qur'ani, Sheikh Qassim amesisitiza kwamba taasisi yake imeanzisha harakati kubwa ya kuimarisha shughuli zinazohusiana na Qur'ani Tukufu, zikiwemo za uchapishaji wa vitabu vya mafunzo ya Qur'ani, dua na pia tafsiri za Qur'ani. Amesema mipango mingine ya taasisi hiyo ni kuboresha mbinu zinazotumika katika ufundishaji wa Qur'ani tukufu nchini Thailand na kuzifanya ziambatane na mifumo ya kisasa kwa sababu mbinu zinazotumika nchini humo hivi sasa ni za zamani na zilizopitwa na wakati. Amesema Taasisi ya Rasuul A'dham ya Thailand imekuwa ikiwasiliana na kuanzisha ushirikiano wa kielimu na taasisi, vutuo na mashirika mbalimbali ya kielimu ya nchi hiyo ili kuboresha viwango vya elimu na masomo ya wanafunzi na wanachuo wa pande mbili.
Katika sehemu nyingine ya mahojiano hayo sheikh Qassim amesema kuwa Jamiatul Mustafa (saw) iliyoanzishwa yapata miaka mitano iliyopita katika mji mkuu wa Thailand Bangkok, imekuwa ikijishughulisha na masuala mbalimbali yanayohusu Qur'ani na kwamba kufikia sasa ina matawi 12 katika mikoa tofauti ya nchi hiyo.
Shughuli nyingi za taasisi hiyo muhimu ya Kiislamu zinahusiana na mafundisho ya Qur'ani, kuarifishwa vitabu muhimu vya Kiislamu, ikiwemo Nahjul Balagha, Sahifatu Sajjadiyah, mafundisho ya fik'hi, itikadi, maadili, akhlaki na hadithi. 640715
captcha