IQNA

Maonyesho ya Ramadhani ya vitabu vya Kiislamu yaanza Lebanon

15:09 - August 25, 2010
Habari ID: 1981212
Maonyesho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ya Vitabu vya Kiislamu yameanza katika mji wa Tripoli wa kaskazini mwa Lebanon.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maonyesho hayo yanafanyika katika kituo cha vijana cha Elimu na Imani cha Jumuiya ya Kiislamu ya Lebanon na yataendelea hadi tarehe 20 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Maonyesho hayo ambayo yanafanyika kwa mwaka wa pili mfululizo yanajumuisha vitabu mbalimbali vya Kiislamu.
Waandalizi wanasema lengo la maonyesho hayo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kuwahimiza vijana wasome vitabu vya Kiislamu.
640211
captcha