Mwandishi wa IQNA nchini Jordan ameripoti kuwa kongamano hilo limehudhuriwa na mhadhiri wa taalumu ya Qur'ani Tukufu Ustadh Ratib Nablisi ambaye alifafanua jinsi ya kufaidika na mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Nablisi amesema kuwa mwezi wa Ramadhani ni fursa kwa ajili ya kufanya mabadiliko katika maisha ya Muislamu na ametoa wito wa kuhuishwa thamani za kiroho za mwezi huu mtukufu.
Ratib Nablisi ameongeza kuwa kwa sasa thamani na matukufu ya kiroho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani hayazingatiwi ipasavyo na kwamba watu wengine wanautumia mwezi huu kwa ajili ya faida za kimaada tu.
Mlinganiaji huyo wa Syria amesisitiza juu ya mchango wa vijana wa Kiislamu katika kukabiliana na changamoto zinazoukabili umma wa Kiislamu na akasema kuwa mwezi wa Ramadhani ni fursa ya kuimarisha zaidi thamani za Kiislamu kati ya tabaka hilo la jamii. 640344