Maonyesho hayo yanaonyesha nakala za kale kabisa za Qur’ani zilizokusanywa kutoka maeneo mbalimbli duniani.
Mbali na nakala za kale za Qur’ani, athari nadra za kale za sayansi na falsafa ya kKislamu pia zinaonyeshwa katika maonyesho hayo.
Vilevile kazi za elimu za nujumu, hisabati na tiba ya Kiislamu ambazo zilikuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya dunia zinaonyeshwa katika maonyesho hayo.
Jumba la Mkumbusho ya Sanaa za Kiislamu la Malaysia ndilo kubwa zaidi katika eneo la kusini mwa Asia na liliasisiwa mwaka 1998 kwa lengo la kuarifisha Uislamu na sanaa za Kiislamu. Jumba hilo lina zaidi ya athari elfu 7 za Kiislamu.
Jumba hilo pia lina maktaba ya aina yake ya sanaa za Kiislamu ambayo ina majmui ya vitabu vya kale na vya sasa vya sanaa za Kiislamu. 642929