IQNA

Maonyesho ya “Umaridadi wa Kaligrafia ya Kiislamu” nchini Indonesia

11:57 - August 29, 2010
Habari ID: 1983010
Maonyesho ya “Umaridadi wa Kaligrafia ya Kiislamu” yanaendelea katika mji mkuu wa Indonesia Jakarta.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, monyesho hayo yaliyoanza tarehe 19 Agosti yanafanyika kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na yanajumuisha athari za kaligrafia za wasanii 10 waliohitimu katika Chuo cha Kaligrafia ya Qur'ani cha Lambaga nchini Indonesia.
Katika maonyesho hayo, mbali na athari za kaligrafia ya Kiislamu vile vile kuna athari za kazi za wasanii waliopata tunzo katika Mashindano ya Saba ya Kimataifa ya Kaligrafia ya Kiislamu yaliyoandaliwa na Kituo cha Utafiti wa Historia, Sanaa na Utamaduni wa Kiislamu chenye makao yake Istanbul nchini Uturuki.
Kaligrafia katika maonyesho hayo ni ile inayohusiana na upambaji vitabu vya Kiislamu, maandishi ya Qur'ani na upambaji wa ndani ya nje ya Misikiti. Maonyesho hayo yataendelea hadi tarehe 22 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
643034
captcha