IQNA

Kuanza kwa duru ya tisa ya mashindano ya Qur'ani Tukufu nchini Tunisia

15:00 - August 30, 2010
Habari ID: 1984065
Duru ya tisa ya mashindano ya kuhifadhi, kusoma na kufasiri Qur'ani Tukufu imekuwa ikiendelea nchini Tunisia tokea siku ya Jumamosi tarehe 28 Agosti.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Saudi Arabia SPA mashindano hayo yanafanyika kwa uungaji mkono wa Rais Zeinul Abideen bin Ali wa Tunisia kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mashindano hayo ambayo yanazishirikisha nchi 21 za Kiislamu na Kiarabu yamefunguliwa na Abubakr al-Akhdhuri, Waziri wa Masuala ya Kidini wa Tunisia. Washindi wa mashindano hayo ya siku kumi watatuzwa na kupewa zawadi baada ya kumalizika rasmi mashindano hayo. 643700
captcha