IQNA

‘Atlasi ya Qurani’ katika maonyesho ya Qurani Tehran

15:19 - August 30, 2010
Habari ID: 1984524
‘Atlasi ya Qurani Tukufu’ iliyotarjumiwa na Mohammad Kermani kutoka Kiarabu na Kiingereza na iliyo na ramani, taswira na tarjuma za aya zaidi ya 1000 kati ya aya za Qurani Tukufu imewasilishwa katika Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Tehran.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA atlasi hiyo inajumuisha maelezo ya Qurani kuhusu maswala kama vile ramani, jedwali na taswira mbali mbali kuhusu maduhui za Qurani za kijiografia, kijamii na kuhustoria. Atlasi hiyo ina kurasa 368 na imechapiswa kwa himaya ya Taasisi ya Quds Razawi.
Maonyesho ya Kimataifa ya Qurani Tukufu ya Tehran yalianza tarehe 27 ya Mwezi wa Shaaban na yataendelea hadi tarehe 23 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. 644483
captcha