IQNA

Rais Ahmadinejad asema mapambano yatawaangamiza maadui wote

15:18 - August 30, 2010
Habari ID: 1984527
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kumeibuka mwamko usio na kifani wa wanamapambano wa mataifa ya eneo kutoka Lebanon hadi Iran jambo ambalo litapelekea kuangamizwa maadui wote.
Akizungmza mjini Tehran alipokutana na maafisa wa ngazi za juu wa Harakati ya Amal ya Lebanon, Rais Ahmadinejad ameongeza kuwa wale wanaopambana dhidi ya maadui wa mwanaadamu na madola ya istikbari wana jukumu zito la pamoja. Rais wa Iran ameashiria mwamko katika ulimwengu wa Kiislamu na kusema mfumo wa kibepari na kibeberu duniani umefika ukingoni na kwamba sasa dunia ina kiu ya utawala adilifu.
644882
captcha