Kwa mujibu wa tovuti ya Euromoney, kikao hicho kimeandaliwa na Shrika la Euromoney kwa madhumuni ya kuchunguza uchumi wa Kiislamu nchini Ufaransa, Ulaya na ulimwengu mzima kwa ujumla. Wanazuoni wa Kiislamu, maafisa wa benki, wakurugenzi wa uwekezaji, wakuu wa bima ya Kiislamu na wawekezaji wa mifumo ya fedha ya Kiislamu watashiriki katika kikao hicho na kuchunguza fursa za kuimarisha uchumi wa Kiislamu nchini Ufaransa pamoja na kustawisha uchumi na sekta ya fedha ya Kiislamu nchini humo.
Kutathminiwa uwezo wa kiuchumi wa Kiislamu barani Ulaya na ulimwenguni na hasa nchini Ufaransa, ikiwa ni kitovu cha uchumi wa Kiislamu barani Ulaya, kusambazwa hundi za Kiislamu nchini humo na kuanzishwa kwa mashirika ya fedha na benki za Kiislamu mjini Paris ni miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa katika kikao hicho cha siku mbili.
Vilevile njia za kushindana uchumi wa Kiislamu na mifumo mingineyo ya kiuchumi, kudhibitiwa migogoro katika mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu na kuunganishwa mfumo wa kiuchumi wa Ufaransa na uwekezaji wa kiuchumi wa Kiislamu ni mambo mengine yatakayopewa uzito katika kikao hicho. 645181