IQNA

Mkuu wa Kituo cha Sanaa za Kiislamu cha Kuwait atembelea maonyesho ya Qur'ani ya Tehran

14:52 - August 31, 2010
Habari ID: 1985419
Mkuu wa Kituo cha Sanaa za Kiislamu cha Kuwait ametembelea kitengo cha watoto cha Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayoendelea mjini Tehran.
Farid al Ali amesema baada ya kutembelea kitengo hicho kwamba ametembelea sehemu mbalimbali za Maonyeso ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran lakini kitengo cha watoto cha maonyesho hayo kina mvuto wa aina yake.
al Ali amesisitiza kuwa watoto wanajifunza mengi katika kitengo hicho, suala ambalo amesisitiza kuwa lina umuhimu mkubwa.
Ameahidi kutembelea tena kitengo cha watoto cha maonyesho hayo kwa ajili ya kujifunza mbinu zinazotumiwa na kuzitumia nchini Kuwait.
Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yataendelea hadi tarehe 27 mwezi mtukufu wa Ramadhani. 645397
captcha