IQNA

Kitabu cha ‘Historia ya Elimu ya Hadithi Mashariki na Magharibi’ chachapishwa na ISESCO

17:50 - September 01, 2010
Habari ID: 1985805
Kitabu cha Elimu ya Hadithi Mashariki na Magharibi mwa Dunia kimechapishwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO.
Kitabu hicho kimeandikwa kwa lugha ya Kiarabu na mhakiki mashuhuri wa Kiislamu wa Mauritania Muhammad al Mukhtar Ould Abah.
Utangulizi wa kitabu hicho umeandikwa na Mkurugenzi Mkuu wa ISESCO Abdul Aziz al Tuwaijri. Ameandika katika utangulizi huo kwamba uchunguzi wa elimu ya hadithi kwa kutumia mbinu za kisasa
umeongezeka katika miongo ya hivi karibuni katika vyuo na taasisi za utafiti wa masuala ya kidini na vituo vya uchunguzi.
Al Tuwaijri ameongeza kuwa elimu ya hadithi ingali inapewa umuhimu na wahakiki na wachunguzi wa mambo na kwamba hii leo kuna idadi kubwa ya wanafikra na wahakiki katika jamii ya Kiislamu wanaofanya juhudi kubwa za uchunguzi na uhakiki katika medani ya elimu za Kiislamu hususan elimu ya hadithi.
Kitabu hicho kina kurasa 745 na kinajadili historia ya elimu ya hadithi mashariki na magharibi mwa dunia. 646326
captcha