IQNA

Shughuli za Qur’ani barani Afrika kuchunguzwa leo katika maonyesho ya Qur’ani ya Tehran

17:54 - September 01, 2010
Habari ID: 1985809
Kikao cha Qur’ani katika Uga wa Kimataifa kanda ya Afrika kinaanza leo saa 12:30 katika maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur’ani yanayoendela mjini Tehran.
Kikao hicho kitachunguza shughuli zinazohusiana na Qur’ani barani Afrika kikihudhuriwa na Naibu Mwenyekiti wa Jamiatul Mustafa al Alamiyya Hujjatul Islam Hakiime Elahi na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Abuja Nigeria Abdul Qadir Mubarak.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa kikao hicho ni katika mfululizo wa vikao vinavyoitishwa na Jamiatul Mustafa al Alamiyya kuhusu shughuli zinazohusiana na Qur’ani katika nyanja za kimataifa.
Kikao kilichopita kilihusu shughuli za Qur’ani katika eneo la Amerika ya Latini na kuhudhuriwa na balozi wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran nchini Mexico Dakta Qadiri Abiyanneh na mshauri wa Jamiatul Mustafa al Alamiyya Hujjatul Islam Rabbani, na balozi wa zamani wa Iran katika nchi za Argentina na Colombia Saadatfar. 646459

captcha