IQNA

Taarifa ya Jumuiya ya Kimataifa ya Amani ya Kiislamu kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds

23:17 - September 02, 2010
Habari ID: 1986169
Jumuiya ya Kimataifa ya Amani ya Kiislamu imetoa taarifa ikiwataka Waislamu wote kushiriki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kuitaja siku hiyo kuwa ni fursa ya kutangaza tena ahadi ya kutetea ubinadamu na amani ya kiadilifu.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa haki za binadamu yaani haki zilizojengeka juu ya dhati ya mwanadamu ni jambo la dharura kwa ajili ya ukamilifu wa kiumbe huyo, kupendana na kuwajibika na ustawi wa maadili mema.
Taarifa hiyo imesema ardhi ya Palestina ni nembo halisi ya kudhulumiwa haki halisi za wanadamu na kukanyagwa sehemu ya mwili wa kiumbe huyo katika kamusi ya historia. “Baadhi wanadai kuwa ni watetezi wa haki za binadamu na wakati huo huo si tu kwamba wanaunga mkono ukandamizaji wa haki za kimsingi za taifa linalokandamizwa la Palestina bali wanausaidia utawala wa Kizayuni wa Israel kutekeleza mauaji ya halaiki dhidi ya watu wasiokuwa na hatia yoyote wa Ukanda wa Gaza na mauaji ya wanachama wa misafara ya misaada ya kibinadamu na wanazuia utekeleza sahihi wa kazi za jumuiya za kimataifa” imesisitiza taarifa hiyo.
Katika sehemu nyingine, Jumuiya ya Kimataifa Amani ya Kiislamu imeashiria hatua ya Imam Khomeini ya kuainisha Siku ya Kimataifa ya Quds na kuongeza kuwa dunia ya sasa inashuhudia maafa makubwa zaidi ya kibinadamu yanayofanywa na Marekani, utawala ghasibu wa Israel na washirika wao katika maeneo mbalimbali. Huko Iraq, Afghanistan, kusini mwa Lebanon na maeneo mengine ya dunia wanadamu wasiokuwa na hatia wangali wananyimwa haki zao za kimsingi za kuishi huku raia wa Gaza wakizuiwa kupata hata misaada ya kibinadamu.
Mwishoni mwa taarifa hiyo Jumuiya ya Kimataifa ya Amani ya Kiislamu imewataka wapigania amani na uhuru, serikali na mataifa ya nchi mbalimbali kuheshimu thamani na utamaduni wa kila upande. Jumuia hiyo pia imewataka watu katika meneo mbalimbali kusihiriki kwenye maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds ya kutetea haki za wananchi wanaokandamizwa wa Palestina. 646117

captcha