IQNA

Kitengo cha tarjumi ya Qur'ani, moja ya vitengo vilivyokuwa na mafanikio maonyesho ya Tehran

14:25 - September 04, 2010
Habari ID: 1986940
Kitengo cha tarjumi za Qur'ani Tukufu cha 'Tarjumane Wahyi' kilikuwa moja ya vitengo vilivyokuwa na mafanikio makubwa katika Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani mjini Tehran.
Kitengo hicho kilikuwa kikitoa taarifa na maarifa kuhusu harakati za tarjumi ya kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu kwa watu waliotembelea maonyesho hayo.
Miongoni mwa huduma zilizotolewa na kitengo hicho ni pamoja ni takwimu za hivi karibuni na taarifa mbalimbali kuhusu harakati ya tarjumi ya Qur'ani Tukufu kwa lugha mbalimbali kote duniani, kuarifisha vituo vya tarjumi ya Qur'ani duniani, kuarifisha tafsiri za Qur'ani za lugha zisizokuwa za Kiarabu na Kifarsi, takwimu kuhusu mchango wa Waislamu wa madhehebu ya Shia na Wairani katika kueneza tafsiri na maarifa ya Qur'ani, ulinganisho wa idadi ya wafasiri wa Qur'ani na waandishi wa taaluma ya kitabu hicho katika kipindi cha karne 14 zilizopita na kadhalika.
Kitengo hicho pia kimeonyesha nakala za tarjumi ya Qur'ani kwa lugha mbalimbali hai na zenye wazungumzaji wengi kama Kiingereza, Kijerumani na Kihispania na lugha za kieneo kama Bisaya, Amazigh na kadhalika. 647187

captcha