Kwa mujibu wa gazeti la Gulf News nuskha hiyo ya Qur'ani yenye upana wa sentimita 14.5 na urefu wa sentimita 24 iliandikwa kwa mkono katika zama za silsili ya Gurkani wakati wa utawala wa serikali ya Aurungzeb mwana wa Shah Jahan ambaye alikuwa muasisi wa jengo maarufu la Taj Mahal.
Kurasa za msahafu huo zimetengenezwa kwa mpunga na mada zinginezo pamoja na kuandikwa kwa wino wa madini yenye thamani.
Imearifiwa kuwa msahafu huo uliandikwa na Aurangzeb na kwamba wakati wa kuandika aliuweka katika eneo maalumu la kasri.
647412