IQNA

Maonyesho ya 'Mwaka wa 1400 wa Kuteremshwa Qur'ani' yafunguliwa Uturuki

12:54 - September 05, 2010
Habari ID: 1987813
Maonyesho ya Mwaka wa 1400 wa Kuteremshwa Qur'ani Tukufu yalifunguliwa jana katika jumba la makumbusho la athari za kale za Kituruki na Kiislamu mjini Istanbul.
Sherehe za ufunguzi wa maonyesho hayo ambayo yataendelea hadi tarehe Mosi Disemba zimehudhuriwa na Mkuu wa Jumuiya ya Masuala ya Dini ya Uturuki Ertugrul Guyan, Waziri wa Utalii Mustafa Çağrıcı, Mufti wa jiji la Istanbul Sophie Makariou, afisa wa kitengo cha Sanaa za Kiislamu cha jumba la makumbusho la Louvre nchini Ufaransa Venetia Porter, naibu mkuu wa jumba la makumbusho ya taifa la Uingereza Filiz Çakır na maulama na wataalamu 250.
Miongoni mwa sehemu muhimu zaidi za maonyesho hayo ni nyaraka nadra zenye kurasa laki mbili na nusu za maandishi ya mkono ya Qur'ani Tukufu ambazo zinanyeshwa kwa mara ya kwanza katika maonyesho hayo.
Nyaraka hizo zinasemekana kuwa za kale zaidi za maandishi ya mkono ya Qur'ani Tukufu. Nyaraka hizo ziliandikwa katika karne ya tisa Miladia.
Athari 1500 za kaligrafia ya Kiislamu pia na athari za kale za Kiislamu za kipindi cha utawala wa kiothmania pia zinaonyeshwa katika maonyesho hayo. Vilevile Qur'ani Tukufu iliyoandikwa na Imam Ali bin Abi Twalib inaonyeshwa katika maonyesho ya Istanbul. 648303


captcha