Kwa mujibu wa tovuti ya All Voices Shirika la Utalii wa Kiislamu ambalo linafungamana na Wizara ya Utalii ya Malaysia, ambalo ndilo limepewa jukumu la kuandaa kongamano hilo limetoa taarifa likitangaza kuwa washiriki 200 kutoka nchi za Iran, Azerbaijan, Brunei, Indonesia, Misri, oman, Saudi Arabia na Afrika Kusini watashiriki katika kongamano hilo.
Tokea sasa kongamano hilo litakuwa likiandaliwa kila mwaka kwa lengo la kuimarisha na kunufaika na suhula za kiutalii zilizoko katika nchi za Kiislamu. Shirika lililotajwa limesema kuwa mbali na washiriki wa nchi hiyo, wawakilishi wengine wa makundi ya kiutalii na viongozi wa kiserikali watashiriki pia katika kongamano hilo.
Shirika hilo limesema kuwa maonyesho maalumu ya utalii katika nchi za Kiislamu pia yatafanyika pambizoni mwa kongamano hilo.
Lengo jingine la maonyesho hayo limetajwa kuwa ni kuimarisha sekta ya utalii ya nchi za Kiislamu na kupambana na athari mbaya za utalii. 649316