Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maonyesho hayo yaliyoanza Septemba Mosi yameandaliwa na Baraza la Kitaifa la Sanaa la Pakistan kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni nchini humo.
Lengo la maonyesho hayo limetajwa kuwa ni kuarifisha thamani za kimaanawi za Uislamu, kuhimiza sanaa ya kaligrafia ya Kiislamu na kuwasaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko nchini Pakistan.
Maonyesho hayo yana athari 150 za wanakaligrafia Waislamu 70 na yanajumuisha kaligrafia ya aya za Qur'ani Tukufu, majina ya Mwenyezi Mungu (Asmaul Husna), jina la Mtume Muhammad (SAW) n.k.
649523