Kazi hizo za sanaa ya Kiislamu ambazo zinaonyeshwa na shirika moja la minada la London, zinajumuisha zaidi ya kazi 30 za sanaa ya Kiislamu za karne tofauti.
Maonyesho hayo yanajumuisha vyombo vya udongo wa mfinyanzi, zana za kivita, bidhaa za kufuma, madini, michoro na maandiko ya mkono ya Kiislamu yaliyokusanywa katika maeneo ya Ulaya, India, Iran, Uturuki, Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika.
Monyesho hayo ambayo ni ya nne kufanyika mjini Doha yatafanyika kwa mnasaba wa sherehe za kuchaguliwa mji huo mkuu wa Qatar kuwa mji mkuu wa utamaduni wa Kiislamu katika mwaka huu wa 2010. 651382