Maonyesho hayo yalifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1910 na mwaka huu yanafanyika kwa mnasaba wa kutimia miaka mia moja tangu yaanze kufanyika.
Maonyesho ya Athari za Kiislamu ya Munich yataendelea hadi mwezi Februari mwakani katika jumba la makumbusho la Munich na maktaba ya mji huo.
Pamoja na mambo mengine maonyesho hayo yatajumuisha vitabu vilivyoandikwa kwa hati za mkono, zana za kivita na mazulia yaliyotengenezwa na wasanii wa Kiislamu.
Athari za kisanii zinazoonyeshwa katika maonyesho hayo zimekusanywa kutoka katika majumba ya makumbusho ya miji mbalimbali ya Ujerumani. 655413