Sherehe za ufunguzi wa taasisi ya Qur’ani na Hadithi ya al Zahra (as) zimefanyika mjini Islamabad Pakistan zikihudhuriwa na hafidhi wa Qur’ani nzima Muhammad Taqi na kwa hotuba ya mkuu wa taasisi hiyo Idris Ahmad Alawi. Sherehe hizo zimehudhuriwa na mamia ya wakazi wa miji ya Islamabad na Rawalpindi.
Sherehe hizo zilianza kwa kiraa ya Qur’ani Tukufu ya mkuu wa Akademia ya Qur’ani ya al Mustafa (saw) Wijahat Hussein.
Mkuu wa taasisi ya Qur’ani na Hadithi ya al Zahra (as) alihutubia hadhara hiyo akisisitiza juu ya umuhimu wa kutolewa mafundisho ya Qur’ani na hadithi.
Amezungumzia vyanzo vya ufuska na tabia chafu kama mamilioni ya mitandao ya intaneti, kanali za televisheni za satalaiti zinazokinzana na maadili bora na utumiaji mbaya wa blututhi na akasema kuwa hali ya kimaadili ya vijana na mabarobaro inatia wasiwasi.
Idris Ahmad Alawi amesema jamii nzima hususan wazazi inawajibika kuwakinga watoto kupitia njia ya kuwafundisha Qur’ani na hadithi. 657842