IQNA

Kuanza mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kwa vijana wa Kiarabu nchini Imarati

17:11 - September 20, 2010
Habari ID: 1997539
Mashindano ya 23 ya kimataifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu na hadithi kwa vijana wa nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi yalianza siku ya Jumapili tarehe 19 Septemba huko Sharja katika Umoja wa Falme za Kiarabu.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Imarati WAM, Jamal al-Hamadi mmoja wa wasimamizi wa mashindano hayo amesema kuwa yanafanyika kwa madhumuni ya kuimarisha thamani za Kiislamu na Qur'ani katika jamii za nchi hizo.
Katika upande wa pili, Khalid al-Yaish, mwakilishi wa sekritarieti ya Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi katika mashindano hayo amesema kuwa kufikia mashindano hayo duru ya 23 kunabainisha wazi jinsi mawaziri wa masuala ya vijana na michezo wa nchi wanachama wa baraza hilo wanavyolipa umuhimu suala la kuzingatia Qur'ani.
Wasimamizi wa mashindano hayo wanasema kuwa wana mpango wa kuanzisha vituo vya kudumu vya kuhifadhi Qur'ani katika misikiti ya miji mbalimbali ya ufalme wa Sharja, vituo ambavyo vitakuwa vikichukua na kuwahudumia wanafunzi wa Qur'ani bila malipo yoyote.
Wanaume na wanawake walio na hamu ya kujifunza Qur'ani watasajiliwa katika vituo hivyo bila kuzingatia umri wao.
Mashindano ya hivi sasa ya Qur'ani na hadithi yameandaliwa na Wizara ya Vijana na Masuala ya Michezo ya Imarati katika Kituo cha Qur'ani na Hadithi za Mtume (saw) mjini Sharjah. Mashandano hayo yamepangwa kuendelea hadi siku ya Alkhamisi Septemba 23. 658608
captcha