Washiriki katika kongamano hilo ambalo litafanyika katika jumba la makumbusho ya Kiislamu la Doha watajadili athari za Kiislamu zilizoko katika jumba la sanaa la Hamad bin Khalifa.
Kongamano hilo lililopewa jina la 'Mwenyezi Mungu ni Jamili Anapenda Umaridadi' litaanza kwa hotuba ya mshindi wa tuzo bora ya usanii ya Pulitzer Paul Goldberger.
Kongamano hilo linahudhuriwa pia na wataalamu wa sanaa kutoka nchi mbalimbali duniani.
Kongamano hilo linasimamiwa na Chuo Kikuu cha Jumuiya ya Madola tawi la Qatar na Taasisi ya Sanaa ya Qatar. Duru ya pili ya kongamano hilo ilifanyika katika mji wa Richmond Virginia Marekani mwaka 2004 chini ya anwani ya 'Mito ya Peponi, Maji katika Utamaduni na Sanaa ya Kiislamu' na duru ya tatu ilifanyika mwaka jana huko Cordoba nchini Uhispania. 658872