IQNA

Mbunge wa kwanza Muislamu wa Australia aapishwa kwa Qur'ani

11:27 - September 29, 2010
Habari ID: 2003806
Mbunge wa kwanza Muislamu katika bunge la Australia aliapishwa jana Jumanne kwa kutumia Qur'ani Tukufu.
Mbunge Ed Husic ambaye wazazi wake walihamia nchini Australia miaka mingi iliyopita aligombea na kushinda kiti cha ubunge kwa tiketi ya Leba katika uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita.
Alisema katika kampeni za uchaguzi huo kwamba anajivunia kuwa Muislamu na kuchukua hatua ya kuapishwa kwa Qur'ani kabla ya kuanza kuhudumia rasmi bunge la nchi hiyo.
Kabla ya hapo Ed Husic alikuwa kiongozi wa jumuiya moja ya wafanyakazi magharibi mwa mji wa Sydney.
Waislamu wanaunda karibu asilimia 2 ya wakazi wote milioni 22 wa Australia. 665367
captcha