IQNA

Kutatuliwa matatizo ya mazingira ya ulimwengu kwa msingi wa mafundisho ya Qur'ani na hadithi

11:32 - September 30, 2010
Habari ID: 2004429
Kikiwa katika siku yake ya pili, kikao cha 15 cha Taasisi ya Aalil Beit (as) ya Jordan kinachofanyika kwa madhumuni ya kujadili maudhui ya Mazingira katika Uislamu, kimejadili masuala mapya yanayohusiana na utatuzi wa changamoto za mazingira kwa msingi wa mafundisho ya Qur'ani, hadithi na sunna za Mtume Mtukufu (saw).
Kwa mujibu wa gazeti la ad-Dastur la Jordan kikao hicho kimechunguza kwa kina mafundisho ya Kiislamu kuhusiana na suala la kulinda mazingira kwa msingi wa mafundisho ya Qur'ani, hadithi na sunna za Mtume (saw) na vilevile mitazamo mipya ya wataalamu na watafiti wa Kiislamu na Kiarabu. Wataalamu mbalimbali wa Kiislamu na Kiarabu wanashiriki katika kikao hicho kilichoanza siku ya Jumanne. 665604
captcha