IQNA

Wafuasi wa dini wakusanyika kulaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani huko Marekani

12:25 - September 30, 2010
Habari ID: 2004463
Wafuasi wa dini mbalimbali walikusanyika jana katika mji wa Minnesota Marekani kwa ajili ya kulalamikia kitendo cha kuvunjiwa heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani nchini humo.
Mkusanyiko huo umetayarishwa na Baraza la Makanisa ya Minnesota.
Wafuasi wa dini mbalimbali waliokutana katika mkusanyiko huo wametangaza upinzani wao dhidi ya hujuma ya hivi karibuni dhidi ya Uislamu nchini Marekani na wakaomba dua ya kuenea hali ya kuheshimiana kati ya wafuasi wa dini mbalimbali.
Kiongozi wa Waislamu wa Minnesota Ja'far Siddiqi alihutubia mkusanyiko huo akisema kuwa Waislamu laki moja na nusu wa mji huo wameathiriwa mno na kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu.
Ameongeza kuwa mahudhurio ya wafuasi wa dini mbalimbali katika mkusanyiko huo pamoja na Waislamu yanawapa Waislamu nguvu zaidi na kukabiliana na hujuma zinazolenga matukufu ya dini yao. 665632
captcha