Kongamano la kieneo la 'Maandishi ya Mkono, Hali Halisi na Mustakbali' litaanza kesho tarehe 3 Oktoba katika mji mkuu wa Oman Muscat. Kongamano hilo linasimamiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESSCO.
Kongamano hilo litafanyika kwa ushirikiano wa Wizara ya Turathi na Utamaduni ya Oman na wataalamu kutoka nchi za Bahrain, Iraq, Misri, Yemen, Libya, Syria na nchi mwenyeji.
Lengo la kongamano hilo limetajwa kuwa ni kupanua maarifa ya watu kuhusu umuhimu wa kulindwa nakala zilizoandikwa kwa hati za mkono na kuzitambulisha kama moja ya nguzo muhimu za utambulisho wa utamaduni na ustaarabu wa Waarabu na Waislamu.
Malengo mengine ya kongamano hilo ni kujadili umuhimu wa kulindwa nakala za mandishi ya mkono za Kiarabu na Kiislamu na utumiaji wa teknolojia ya kisasa kwa ajili ya kuhifadhi nakala hizo na vilevile kutoa elimu na maarifa kuhusu hali ya nakala za maandishi ya mkono katika nchi za Kiarabu.
Pambizoni mwa kongamano hilo kutafanyika maonyesho ya nakala za maandishi ya mkono. 666814