Hadi Aziz Zadeh, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO anayeshughulikia masuala ya utamaduni, amezungumzia suala la kuzinduliwa hivi karibuni mjini Tehran Sekretarieti ya Wanawake Wasomi wa Ulimwengu wa Kiislamu.
Akiashiria suala hilo katika mazungumzo yake ya hivi karibuni na Kamran Daneshjuu, Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Iran, Aziz Zadeh amesema kuwa kitengo maalumu cha kushughulikia masuala ya wanawake wasomi wa Kiislamu kimefunguliwa katika idara kuu ya Isesco na kwamba sekretarieti yake itakuwa mjini Tehran.
Aziz Zadeh amemwalika Daneshjuu kushiriki katika kikao cha tano cha Mawaziri wa Elimu ya Juu na Utafiti wa Kielimu wa nchi za Kiislamu ambacho kimepangwa kufanyika hivi karibuni huko Kuala Lumpur nchini Malaysia. 666931