IQNA

Mkutano wa mawaziri wa mazingira wa OIC kuanza leo

10:55 - October 05, 2010
Habari ID: 2006876
Mkutano wa mawaziri wa mazingira wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC unaanza leo nchini Tunisia chini ya usimamizi wa Rais Zainul Abidin bin Ali wa nchi hiyo. mkutano huo utaendelea kwa muda wa siku mbili.
Mkutano huo umetayarishwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la nchi za Kiislamu ISESCO, Kituo cha Hali na Hewa na Ulinzi wa Mazingira cha Saudi Arabia, sekretarieti ya OIC, na Wizara ya Mazingira na Ustawi Endelevu ya Tunisia.
Mawaziri wa mazingira wa nchi 57 wanachama wa OIC na viongozi wa zaidi ya jumuiya 30 za kimataifa za Kiislamu zinazoshughulikia mazingira wanahudhuria mkutano huo. Mawaziri hao wanajadili masuala yanayohusiana na mazingira katika ulimwengu wa Kiislamu.
Washiriki katika mkutano huo pia watabadilishana mawazo kuhusu hati mbili muhimu za 'fremu ya mipango ya kazi za Kiislamu kuhusu ustawi endelevu' na 'ratiba ya kazi za Kiislamu kwa ajili ya kustafidi na mifuko wiano'.
Mkutano huo pia utachunguza ripoti, nyaraka na stratijia za jumuiya mbalimbali za mazingira ikiwa ni pamoja na ripoti ya shirika la ISESCO kuhusu ulinzi wa mazingira, uendeshaji wa vyanzo vya maji, nishati jadidika na ustawi endelevu. 668438

captcha