Shirika rasmi la habari la Sudan limeripoti kuwa kongamano hilo linafanyika katika kutekeleza kivitendo maazimio ya mkutano wa OIC uliofanyika Makka na mipango ya miaka 10 ya jumuiya hiyo kuhusu usalama wa chakula.
Katibu wa kongamano hilo Abdullah Ahmad Othman amesema kuwa wawakilishi wa nchi 57 wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC, nchi nne wanachama waangalizi, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Nchi za Kiislamu, Umoja wa Afrika, Benki ya Kimataifa, Shirika la Kimataifa la Chakula FAO, Benki ya Ustawi ya Kiislamu na jumuiya 35 za kimataifa watashiriki katika kongamano hilo.
Amesema kuwa Sudan imechaguliwa kuwa mwenyeji wa kongamano hilo kutokana na kuwa nchi hiyo pia ilichaguliwa katika mkutano wa Kimataifa wa Roma kwa ajili ya kushiriki kwenye mapambano ya kukabiliana na mgogoro wa uhaba wa chakula duniani. 668979